Al-Qur'an Al-Kareem

Muhammad (PBUH)

Announcements

Events

Partners

Home

Donate

 

Sheikh Muhammad Sayyid Tantawi afariki dunia

إِنَّا لِلّهِ وَإِنَّـا إِلَيْهِ رَاجِعونَ

Sheikh Mkuu wa Tanzania Sheikh I ssa Shaabani Simba (shoto) akiwa katika picha ya pamoja na Sheikh Mkuu wa Misri (Sheikhul-Azhar - GRAND SHEIKH OF AL-AZHAR - Pr,) Dr Muhammad Sayyid Tantawi katika Ofisi yake mwezi uliopita.

Sheikh Mkuu wa Tanzania alikuwa nchini Misri kuhudhuria Mkutano Mkuu wa 22 (The 22nd General Conference. Under the Title The Objectives of Shariah (Islamic Law) And Issues of the Contemporary Age.

Marehemu amefariki Jumatano ya tarehe 10/03/2010 (24 Raby' Al-Awwal 1431 A.H.) asubuhi katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Riadh nchini Saudi Arabia akijiaanda kwa safari ya kurudi nchini Misri. Mara baada ya kupatwa na mshtuko wa moyo, Sheikh alikimbizwa katika hospitali ya King Khaled military hospital ambapo alipofariki dunia. Sheikh alikuwa nchini Saudia Arabia kuhudhuria hafla ya ugawaji wa tunzo ya Mfalme Faisal iliyokuwa ikigaiwa kwa baadhi ya viongozi kutoka nchi mbalimbali akiwemo Waziri Mkuu wa Uturuki.

Sababu za kifo chake ni Presha (Mshtuko wa Moyo) uliomtokea ghafla akiwa kwenye ngazi ya ndege. Taarifa zinasema hali hiyo imetokana na uchovu aliopata kutokana na shughuli hiyo ya jana.

اللهم اغفر له وارحمه

Zingatia: hakikisha kompyuta yako ina 'support' maandishi ya kiarabu kwa kusoma maandishi yaliyoandikwa kwa kiarabu kwenye website hii.

 

 
 
 

:::: © Salama Charitable Trust ::::